Karibu kwenye mwongozo wetu wa mtumiaji
Ingawa tumejitahidi kuifanya iwe rahisi sana, hapa kuna mwongozo mfupi wa kukusaidia kupitia mchakato wa kuhariri.
Bana Picha
Ili kubana picha, chagua hati kutoka kwenye kifaa chako, akaunti ya Google Drive au Dropbox. Faili zitabanwa hadi kufikia ukubwa mdogo zaidi iwezekanavyo huku zikihifadhi ubora wa juu zaidi. Baada ya kuchakatwa, unachopaswa kufanya ni kupakua picha zako zilizobanwa au kuzituma tena kwenye akaunti zako za wingu.
Badilisha Ukubwa wa Picha
Ili kubadilisha ukubwa wa picha, zichague kutoka kwenye kifaa chako, akaunti ya Google Drive au Dropbox. Utaona onyesho la ukaguzi la picha zako likiwa na ukubwa wa awali wa faili. Ukijaribu kubadilisha ukubwa wa picha zenye vipimo tofauti huku ukidumisha uwiano halisi, thamani za upana na urefu utakazoingiza zitazingatiwa kama thamani za juu pekee. Unaweza kuangalia thamani za mwisho za upana na urefu chini ya onyesho la ukaguzi la kila picha. Kisha, pakua picha zako zilizobadilishwa ukubwa au uzitume tena kwenye akaunti zako za hifadhi ya wingu.
Punguza Picha
Ili kupunguza ukubwa wa picha, chagua kutoka kwenye kifaa chako au akaunti ya Google Drive au Dropbox. Utaona onyesho la ukaguzi la picha zako. Ikiwa unataka kupunguza picha moja, unaweza kufanya hivyo mwenyewe kwa kurekebisha fremu kuzunguka sehemu unayotaka kupunguza. Ukichagua kundi la picha za kupunguza, unaweza kupunguza kwa uwiano wa kawaida wa picha (3:2, 4:3, 5:4, 1:1, 4:5, 3:4, 2:3). Baada ya kupunguza ukubwa, unaweza kubadilisha ukubwa wa picha zako ili kupunguza ukubwa wa faili ikiwa itahitajika.
Badilisha kuwa JPG / Badilisha kutoka JPG
Ili kubadilisha kuwa JPG au kutoka JPG, chagua tu faili kutoka kwenye kifaa chako, akaunti ya Google Drive au Dropbox. Utaona vijipicha vya picha zako. Unapopakia JPG, unaweza kuibadilisha kuwa PNG au GIF. Unaweza pia kubadilisha picha za TIF, PNG, GIF na RAW kuwa muundo wa JPG. Baada ya hapo, bofya badilisha na pakua faili zako au uzihifadhi tena kwenye akaunti zako za wingu.
Zungusha Picha
Ili kuzungusha picha zako, zichague kutoka kwenye kifaa chako, akaunti ya Google Drive au Dropbox. Kisha bofya aikoni ya ili kuzizungusha katika upande unaopendelea. Unaweza kuchagua picha za muundo wa mlalo au wima pekee. Zana hii ni muhimu sana kwa ajili ya kuzungusha makundi ya picha kwa kubofya mara moja tu.
Tengeneza GIF iliyohuishwa
Tumia zana yetu ya 'Badili kutoka JPG' ili kutengeneza GIF yako iliyohuishwa. Chagua zaidi ya faili moja ya JPG kutoka kwenye kifaa chako, akaunti ya Google Drive au Dropbox. Utaona muonekano wa awali wa picha zako. Kisha weka idadi ya sekunde kwa kila picha na uchague kama unataka GIF ijirudie au la. Mwishoe, bonyeza badili na upakue GIF yako iliyohuishwa.
Kupanga faili
Unaweza kupanga faili zako upendavyo. Bofya tu kwenye vijipicha vya picha zako na uziburute ili kuziweka mahali ulipochagua. Pia unaweza kuzipanga kwa kufuata alfabeti au kinyume chake.
Kasi ya upakiaji na uchakataji
Muunganisho wa Intaneti ulio na kasi ndogo na faili kubwa unaweza kuathiri kasi ya kupakia na kuchakatwa. Ikiwa kivinjari chako kitakumbana na kukatizwa wakati faili inachakatwa, utakuwa na uwezo wa kuangalia hali ya kuchakatwa kwenye ukurasa wa “Faili Zilizochakatwa karibuni” kwenye Akaunti yako.
Inapakua
Faili zako zilizochakatwa zitabaki kwenye seva zetu ili kukupa muda wa kutosha wa kuzipakua. Kulingana na aina ya akaunti yako, zitatunzwa kwa muda kati ya saa 1 hadi 2. Hata hivyo, unaweza kufuta faili lako mara tu baada ya mchakato wa kubadilisha kukamilika kwa kubofya aikoni ya () .
Inafanya kazi kutokea kwenye wingu
Faili unazotaka kuchakata hazihitaji kuhifadhiwa kwenye kifaa kile kile unachotumia. Hii ina maana kwamba ikiwa una akaunti ya Google Drive au Dropbox, unaweza kupakia faili zako moja kwa moja kwenye ukurasa wetu. Baada ya faili zako kuchakatwa, unaweza kuzihifadhi tena kwenye akaunti zako za wingu. Huduma hii inaweza kusaidia hasa unapotumia iLoveIMG kwenye simu au kishikwambi.
Chagua faili za kupakia
Kuna njia mbili za kupakia picha zako haraka. Unaweza kuburuta na kudondosha picha zako kutoka kwenye kompyuta yako moja kwa moja hadi kwenye ukurasa wetu. Au unaweza kuchagua picha zako kwa kuzibonyeza moja baada ya nyingine. Ili kuchagua picha nyingi kwa pamoja zikifuatana, bofya picha ya kwanza na ya mwisho unazotaka huku ukiwa umeshikilia kitufe cha 'Shift'.
Matatizo Mengine
Toleo jipya la iLoveIMG limeundwa ili kuhakikisha utendaji kazi mwepesi na kuboresha uzoefu wako kama mtumiaji. Hata hivyo, ukikumbana na tatizo lolote au ukipenda kutupatia maoni yoyote, tafadhali jisikie huru kututumia barua pepe. Tutafurahi kukusaidia.